Tamko la CEMOT kuhusu hali ya Uchaguzi na Utoaji Matokeo

28.10.2015



CEMOT imefuatilia kwa ukaribu jinsi utaratibu wa kutoa matokeo unavyoendelea.

  1. Hadi sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa taarifa za majimbo zaidi ya 220 ambayo ni zaidi ya asilimia 80%
  2. Akinukuliwa na vyombo vya habari, mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa ametangaza kuyakataa matokeo yote yaliyotangazwa na NEC. 
  3. Kwa upande wa Zanzibar, Mwenyekiti wa wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) ametangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi ya Urais wa Zanzibar.
Hivyo basi

  1. Tunaihimiza NEC kuharakisha kutoa matokeo ya majimbo yaliyosalia ili kupunguza hali ya sintofahamu kwa watanzania wanaosubiri kufahamu hatima ya kura zao walizopiga toka tarehe 25 Oktoba 2015
  2. Utaratibu wa kukataa matokeo ni vyema ukafanywa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za Uchaguzi zilizowekwa.
  3. Hali ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar kunahitaji kufafanuliwa kwa wananchi ili ueleweke na kuondoa wasiwasi uliotanda kuwa kitendo hicho kinaathiri uchaguzu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  4. Kuendelea kusikiliza na kutolea ufafanuzi masuala ya kisheria na taratibu yanayoonekana kuibuka kipindi hiki cha kutangaza matokeo ikiwa ni pamoja na yale yanayoibuliwa na washindani
Kiujumla

  1. Tunapenda kuwapongeza watanzania kwa uvumilivu, utulivu na busara wanayoitumia wakati wa kusubiri na kupokea matokeo
  2. Tunapenda kusisitiza kuwa amani ya Tanzania iko mikononi mwa Watanzania na kila Mtanzania anao wajibu wa kulinda amani kwa manufaa ya Watanzania na dunia kwa ujumla
  3. Tunawaomba wadau wote wa uchaguzi hususani vyama vya siasa, wagombea wa nafasi mbalimbali kuendelea kuheshimu sheria na utawala wa sheria na kuepuka kutoa matamko yanayoweza kusababisha kutoweka kwa amani na utulivu katika jamii. Aidha tunawashauri wadau wa uchaguzi kutumia njia ya mazungumzo au kutafuta haki kupitia vyombo vya sheria badala ya kutoa matamko yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi.


Imetolewa na CEMOT
Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel, Dar es Salaam
Tarehe 27, Oktoba 2015

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger TemplatesPublished.. Blogger Templates