Kitendo cha kuchana picha za mgombea sikizuri kwa ni kinavunja sheria na kanuni za tume ya uchaguzi. Pia kinaweza kuzusha na kuleta mtafaruku.
Katika uchaguzi wa kidemokrasia kwa nchi yoyote ile uvumilivu na kuepuka uchokozi wa aina yoyote ndiyo nguzo ya zoezi hilo kufanyika kwa amani na utulivu.
Ieleweke kuwa,chumba cha kupigia kura ndiyo mahali sahihi ambapo mpiga kura anaweza kuelezea hisia zake kuhusuc hama au mgombea fulani kwa kupiga kura kwani uchaguzi ni kupiga kura sio kuchana mabango.
Vile vile, mabango ya mgombea kubandikwa kwenye nyumba za serikali kama inavyoonekana kwenye picha ni makosa makubwa. Ikumbukwe kuwa, nyumba za serikali ni za umma. Kwahiyo, kutumika kama sehemu ya kubandika matangazo ni kukiuka kanuni na taratibu za uchaguzi.
Mambo yote mawili yanaweza kuleta au kuibua hisia za watu na kusababisha vurugu ama vitendo vingine vyenye kuashiria uovu.
No comments: