Kituo cha uangalizi wa uchaguzi "Muhtasari #4



Utangulizi
Kituo cha uangalizi wa uchaguzi kinakusanya taarifa za mchakato wa uchaguzi kutoka nchi nzima. Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, waangalizi wetu zaidi ya mia tatu wanawasilisha taarifa zinazotuwezesha kutambua mwenendo wa uchaguzi, matukio ya pekee na madhara yanayoweza kutokana na matukio hayo. Waangalizi wetu wamesambaa katika majimbo yote 265 Tanzania Bara na Zanzibar ambapo wanatutumia taarifa kila siku.

Waangalizi wetu wanafuatilia mikutano miwili kila siku inayoweza kuwa ya wabunge, madiwani au urais. Taarifa zinazokusanywa zinajikita kwenye maeneo makuu sita ambayo ni mwenendo wa vyama siasa, utendaji kazi wa Tume za uchaguzi, uwepo na utendajo wa jeshi la polizi, ushiriki wa makundi maalumu, usalama na elimu ya mpiga kura. Kwa siku mbili zilizopita, waangalizi wetu wametembelea vituo mbalimbali vya kupiga kura, kushuhudia maandalizi ya uchaguzi.

Uchambuzi huu unatokana na taarifa tulizozipokea kutoka 25/9/2015 and 24/10/2015, kutoka kwa waangalizi 301 katika majimbo 229 Tanzania bara na Zanzibar.

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger TemplatesPublished.. Blogger Templates