Kukosekana kwa majina ya wapiga kura kunaweza kusabablisha vurugu wakati wa uchaguzi


Na Ruth Meena
Mkurugenzi wa Baraza la Habari ndugu Kajubi Mukajanga akiwa kwenye mahojiano na Radio One, (22.10.2015) amehimiza Tume ya Uchaguzi kushughulikia tatizo la kukosekana kwa majina ya wapiga kura katika daftari la wapiga kura. Baadhi ya majina yanayokosekana ni pamoja na la kwake mwenyewe, waandishi wa Habari na Mgombea kiti cha Udiwani. Kukosekana kwa majina ya watu katika daftari la wapiga kura, ikiwa ni pamoja na wagombea katika nafasi mbalimbali, waandishi wa habari na watu wengine halitachukuliwa kama ni tatizo la kawaida la kiufundi. Litapewa taswira ya kisiasa hivyo kuwezekana kusababisha vurugu wakati na baada ya chaguzi. Tatizo hili lisipuuzwe kwani linaweze kusababisha vurugu wakati na baada ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi itafute mbinu stahiki za kushughulikia hili tatizo haraka iwezekanavyo kwa siku hizi zilizobakia.

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger TemplatesPublished.. Blogger Templates