Amb. Dr. Ahmed Kiwanuka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa taarifa kwa umma kuhusu adhabu ya kukiuka maadili aliyopewa mgombea mwenza wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Juma Duni Haji. Hata hivyo taarifa hiyo imepokelewa kwa hisia kali dhidi ya NEC. Kwa namna siku ya uchaguzi ilivyokaribia huenda ikaonekana kama lengo ni kuumiaza upinzani.
Ni wazi kuwa yapo makosa yamefanywa na vyama vingine kama CCM ikiwemo kutoa lugha chafu zinazokera hasa matusi, kejeli nk. NEC haijasema lolote. Kwa mantiki hiyo uamuzi dhidi ya CHADEMA au UKAWA unaweza kuzaa neema ya huruma upinzani.
Ikumbukwe kuwa kuna kura zingali zinaelea. Kura hizo ni zile za jazba na huruma. Ikiwa NEC itaonekana kupendela, kura za aina hiyo zikaamini upo upendeleo basi kuna uwezekano wa NEC na CCM kuadhibiwa na wapiga kura wanaoelea. Katika duru za uchaguzi kura moja ni muhimu isidharaulike kwani anaeipata kheri, anayeipoteza balaa kwani milioni huanza na moja.

Picha za taarifa hiyo:
No comments: