Maandalizi ya NEC


  • Idadi ya ripoti za waangalizi zinazoashiria kukamilika kwa maandalizi ya uchaguzi zinazidi kuongezeka

Majumuisho na hitimisho

  • Waangalizi wetu wameshuhudia mikutano 3,814 ya kampeni za vyama
  • Ripoti za waangalizi zinaonesha ongezeko la elimu ya mpigakura kadri uchaguzi ulivyokaribia
  • Asilimia ndogo ya wagombea ubunge ni wanawake, hasa kwa vyama vyenye wagombea wengi, kwa mfano CCM (9% wanawake) na CHADEMA (6%).
  • Zaidi ya nusu ya wapigakura walioandikishwa ni wanawake (53%)
  • Zaidi ya nusu ya walioandikishwa na NEC ni vijana chini ya miaka 35 (57%)
  • Kuna ripoti chache tu za unyanyasaji wa kijinsia wakati wa kampeni, katika siku sita za uangalizi
  •  Ripoti za waangalizi zinaonesha kwamba hakuna mabadiliko katika kutii au kutotii miongozo na taratibu za uchaguzi kwa upande wa vyama
  • Idadi ya ripoti za waangalizi zinazoashiria kukamilika kwa maandalizi ya uchaguzi zinazidi kuongezeka

Kwa ujumla, taarifa hizi zinaonesha kwamba nchi yetu ipo tayari kwa uchaguzi, ingawa kumekuwa na changamoto za hapa na pale.

Tunahimiza Watanzania watumie haki yao ya kupiga kura, na tunaitakia nchi yetu uchaguzi mwema.

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger TemplatesPublished.. Blogger Templates