Matusi katika siasa: Je ni utamaduni wa siasa tunaotaka kujenga taifa letu?


Na Ruth Meena


Mijadala ya wanao wania nafasi za uongozi inapotawaliwa na matusi inaonesha kutopevuka kwa siasa na wanasiasa wetu. Kwa hali ambayo sio ya kawaida, mwanasiasa mashuhuri alinukuliwa akisema, wanaume wanaotaka mabailiko wabebe mimba! Wanaume kubeba mimba maana yake ni nini? Je, wanawake wanaodai mabadiliko wafanye nini?
Wanasiasa wanapo filisika kuwa na nguvu za hoja, wanyamaze, maana maneno kama hayo yanavunja utu wataifa letu, yanavunjia wanawake heshima, nani aibu kwa wale wote wanotetea utu wataifa. 

Taarifa nyingi zinaotoka kwaWaangaliziwa Kituo cha Uchaguzi (uchaguziwetu2015) zinaonesha kwamba wanaojinadi kwa wapiga kura mara kwa mara hawanadi sera bali wanachukua nafasi za majukwa akutukanana. Je, kwa hili Tume ya Uchaguzi ya Taifa haina miongozo kuhusu lugha halali kwa wagombea? Zinapo baki siku chache kukaribia uchaguzi, wanasiasa wangetumia muda huu, kuimarisha sera zao ili wapiga kura waweze kuchagua sera. Mijadala ya matusi ina wanyima fursa wapiga kura kuchagua kwa usahihi na kupotezea wapiga kura muda wanaotumia kuwa sikiliza wanaojinadi.

Tazama Video hio hapa chini.


Mgombea wa Udiwani Kaliua Tabora akinadi sera kwa lugha ya kashfa


No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger TemplatesPublished.. Blogger Templates