Tamko la CEMOT kuhusu zoezi la kutangaza matokeo linaloendelea

Oktoba 27, 2015

Kituo cha Uangalizi wa Uchaguzi (CEMOT) kimepokea taarifa mbalimbali kutoka kwa waangalizi wake wapatao 10,050, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ndani na nje ya nchi zinazogusa zoezi zinaloendelea la kuhesabu na kutangaza matokeo.
  1. Katika maeneo mbalimbali, hasa katika ngazi ya ubunge, kuna taarifa za kuchelewa kutolewa kwa matokeo. Hadi sasa majimbo zaidi ya 150 yamesha toa majibu. Hii ni zaidi ya asilimia 50. Baadhi ya maeneo ambayo pamoja na Arumeru Magharibi, Mbagala, Kawe, Kibamba. Pia kuna taarifa kutoka baadhi ya majimbo kama ambapo baadhi ya wagombea walioshindwa wamekataa kusaini fomu za matokeo. 
  2. Kumekuwa pia na malalamiko toka kwa Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia UKAWA, Edward Lowassa kuhusu Tume kutangaza matokeo ya urais kwa kufuata majimbo ambayo CCM imeshinda. Kwa mujibu wa Lowassa, huo ni mkakati wa kuwaanda wananchi kisaikolojia kukubali matokeo na kuitaka Tume itoe matokeo kwa ujumla wake. Akiongea wakati wa kutoa matokeo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa ametoa mwongozo kuwa Tume inatangaza matokeo kwa jinsi yanavyoingia.

Kwa kiasi kikubwa Tume imekuwa imeonekana kufanya kazi zake kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi katika kufanya kazi zake.

Katika ngazi ya ubunge hasa maeneo ambayo zoezi la kuhesabu kura limekamilika, ni vyema maafisa uchaguzi wa maeneo husika watoe matokeo haraka au kubainisha sababu za kuchelewesha matokeo hayo ili kuondoa hali ya mashaka na sintofahamu miongoni mwa jamii. Kwa kufanya hivyo, kupunguza vurungu zisizo na lazima kwani wananchi wanaposubiri kwa muda mrefu, wanaanza kuhisi kuwa haki yao inataka kupokonywa.

Kwa kutambua mchango wa waandishi na wachambuzi mbalimbali wa masuala ya uchaguzi wa ndani na nje ya Tanzania, ni vyema waandishi na wachambuzi wakatjikita katika kutoa taarifa zilizothibitishwa na zenye uchambuzi wa kina ili kuweza kuimarisha umoja wa taifa letu.

Watanzania katika maeneo mengi wameendelea kuonesha utulivu wa hali ya juu ingawa kuna maeneo yenye vurugu. CEMOT inaamini kuwa yale maeneo ambayo kumekuwa na vurugu ni vyema vyombo vya usalama hususan Polisi vikaimarisha ulinzi unaozingatia haki za raia. CEMOT inapongeza utendaji wa Jeshi la Polisi kwa weledi ulioonesha katika kusimamia zoezi zima la uchaguzi.


Imetolewa na CEMOT
Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel, Dar es Salaam
Tarehe 27, Oktoba 2015

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger TemplatesPublished.. Blogger Templates