Mchakato wa Uchaguzi
Chanzo: International IDEA
1.2 Wadau wakuu kwenye kutekeleza mchakato wa uchaguzi
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Wizara mbalimbali hususani ya sheria, wanawake na watoto, polisi, takukuru na Tume ya Haki Za Binadamu, asasi za kiraia Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya Siasa, na Polisi. Kazi kuu ya Tume ni pamoja na kuratibu wadau wahusika katika kusimamia utekekezaji wa mpango kazi wa mchakato kabla ya uchaguzi, wakati wa kupiga kura, kutoa tamko rasmi la matokeo, kuchambua mchakato na kuanza mchakato wa uchaguzi unaofuata.
1.3 Misingi inayoongoza utendaji wa Tume za Uchaguzi
Tume za Uchaguzi hufanya kazi kwa kuongozwa na mfumo wa sheria zilizoko hususani za kulinda haki za wanawake na wanaume katika uchaguzi. Hii ni pamoja na: Katiba, Sheria za nchi, mikataba ya kimataifa kuhusu haki za wanawake na wanaume katika ushiriki kama wapiga kura, wanaowania nafasi mbalimbali za uwakilishi, wenye ulemavu, wazee na vijana. Mfumo huu ni kama unaelezwa
na mchoro ufuatao.
1.4 Majukumu ya Tume kwenye mchakato wa uchaguzi
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (1977) Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepewa majukumu yafuatayo;
Kabla ya kupiga kura:

- Kusimamia na kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura kwaajili ya Uchaguzi wa Urais, Ubunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Kusimamia na kuendesha Uchaguzi wa Rais na Ubunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Kupitia mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika majimbo mbali mbali ya Uchaguzi wa Ubunge.
- Kusimamia na kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura na kuendesha Uchaguzi wa Madiwani.
- Kutangaza matokeo ya Viti Maalum vya wanawake vya Ubunge na Udiwani.
- Kutoa Elimu ya Mpiga Kura na kusimamia Watu na Asasi zitazokazohusika katika Kutoa Elimu hiyo.
- Kutekeleza Majukumu mengine yatokanayo na sheria zilizotungwa na Bunge.
Kabla ya kupiga kura:
- Kusimamia misingi ya kuwezesha uchaguzi huru na haki kwa mrengo wa jinsia
- Uchambuzi yakinifu wa mfumo wa sheria, kubaini vikwazo vitokanavyao na sheria katika kuwezesha ushiriki wa wanawake na wanaume katika mchakato kwa kuzingatia sheria za nchi, mikataba ya kimataifa na kikanda, na katiba ya nchi.
- Kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili kuhaikisha uchaguzi huru na wa haki yenye mengo wa jinsia
- Kuratibu elimu ya uraia na ya wapiga kura na kuhakikisha inalenga makundi yote
- Kuhakikisha ajira ya watendaji katika mchakato unazingatia misingi ya usawa wa jinsia
- Kusimamia uandikishaji wa wapiga kura unaowezesha makundi yote kujiandikisha
- Kubaini vituo vya uandikishaji na vya kupiga kura vifikiwe na makundi yote kwa kuzingatia ushiriki wa wanawake, na makundi ya pembezoni
- Kutoa miongozo, taratibu, miongozo ya maadili kwa watendaji wote, itakayoongonza uzingatiaji wa sheria wakati wa mchakato zinazowezesha ushiriki wa makundi yote (guidelines, codes of conduct, regulations)
- Kutoa miongozo kwa vyombo vya habari ili kuhakikisha vinazingatia sheria, maadili na kuwezesha ufikiaji wa wanaowania nafasi mbalimbali katika mchakato
- Kuratibu kampeni ili kuhakikisha wagombea wote wanaongozwa na sheria, kutokupendelea upande wowote, na kuhakikisha watendaji wengine kama vile polisi, vyombo vya usalama vinatimiza wajibu wao bila upendeleo
- Kutoa miongozo kwa wafuatiliaji wa ndani na nje inayowezesha wafuatiliaji wanafanya kazi yao kwa kuzingatia sheria zitokanavyo na misingi ya haki na uhuru Wakati wa kupiga kura:
- Kuhakikisha usalama wa wapiga kura
- Kuhakikisha wasimamizi wanafanya shughuli zao kwa kuzingatia maadili, miongozo na taratibu zilizokubalika
- Kupokea malalamiko yatokanayo na ukiukwaji wa miongozo na kuishughulikia mara moja
- Kusimamia kuhesabu kura
- Kutangaza matokeo Baada ya kupiga kura:
- Kupokea ripoti za watazamaji/waangalizi wa ndani na nje
- Kutathmini mchakato wa uchaguzi
- Kuanza mpango kazi kwa ajili ya mchakato mwingine
No comments: