Na Ruth Meena
Kumekuweko na malumbano kuhusu kulinda kura wakati wa kuzihesabu. Ingawaje jambo hili linaonekana dogo, linaweza kuliingiza taifa kwenye machafuko wakati wa zoezi la kuhesabu kura. Suala la kujiuliza ni hili: ni kitu gani kinachosababisha madai ya kulinda kura katika muktadha ambao kila chama kilichoshiriki kinakuwa na wakala wake kwenye vituo vya kupiga na kuhesabia kura? Na suala la pili, ni kitu gani kinachosababisha wale wanaopenda kulinda kura zao wakati wa zoezi la kuhesabu kura wanyimwe kufanya hivyo hata kama sheria inawaruhusu? Tukumbuke kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2010, katika jimbo la Ubungo vijana wa Chadema waliamua kukesha kwa takribani wiki moja wakihofu kuchakachuliwa kwa matokeo.
Kitendo hiki kilifanywa kwa amani na mara chache polisi waliokuwa kwenye lindo walionekana wakijiunga kwenye nyimbo za amani. Kipindi hiki kulikoni?
Ulinzi wa kura unatokana na sababu kadhaa. Kwanza kabisa unatokana na baadhi ya wadau wa uchaguzi kukosa imani na mfumo wa kusimamia shughuli za uchaguzi. Hoja za kambi ya upinzani ni kuwa Tume ya Uchaguzi haiko huru, haina uwezo wa kuhakikisha kuwa uchaguzi ni huru na wa haki, na kwamba chama tawala kinaweza kutumia mamlaka yake kushawishi uchakachuaji wa kura. Hoja za serikali ni kwamba makundi ya ulinzi kwenye vituo vya kuhesabia kura yanaweza kusababisha vurugu, hivyo kuyakataza ni njia moja ya kuhakikisha usalama wakati wa kupiga na kuhesabu kura.
Pande zote mbili zina hoja zenye mantiki. Hata hivyo, kuzuia ulinzi wa kura kunaweza kusiwe ni suluhisho la kuliepusha taifa na vitendo vitakavyoashiria uvunjaji wa amani katika kipindi hiki. Uchaguzi wa mwaka huu ni wa ushindani mkubwa. Tumeshuhudia vitendo vya hapa na pale vilivyosababisha uvunjaji wa amani. Mwaka huu, vijana wengi wamehamasika sana kujiandikisha kupiga kura, takribani nusu ya wapiga kura wote ni vijana kati ya miaka 18-35. Kundi kubwa la hawa vijana linadai mabadiliko na hivyo wengi wamejiunga na kambi ya upinzani wakiamini kuwa neema itawajia. Wengi wa vijana hawa ni wale wanaoishi maisha yanayowapambanisha na polisi kila siku, kama vile waendesha pikipiki, bajaji au machinga. Polisi watakapotumia nguvu ya ziada kupambana nao wajue kuwa vijana wengi hawaogopi kupambana nao kwani ndiyo maisha wanayoishi kila siku. Hili ndilo kundi linalotegemewa kukesha kulinda kura. Hawa ndio watakaopoteza maisha ikiwa polisi watalazimika kutumia vyombo vya moto kuwasambaratisha.

Sisi ni mashuhuda wa machafuko yaliyokwisha tokea kwa majirani zetu. Hivi karibuni huko Burundi tumeshuhudia maelfu ya vijana kupoteza maisha yao, kina mama na watoto wakikimbia na wengine kujeruhiwa au kuuwawa, lakini wale wahusika wakuu waliosababisha fujo wanabaki na ulinzi mkubwa au wanakimbia kwa njia ya ustaarabu na kupata hifadhi za heshima kwa wenyeji wao. Kwenye hili kinachotakiwa hapa ni hekima, wala siyo nguvu au jaziba. Viongozi wa pande kuu zenye ushindani wa kisiasa wanahitaji wakubaliane juu ya njia nzuri na ya wazi itakayotumika kuhesabu kura ili kujenga imani kuhusu hesabu za kura. Ushindani wa CCM na UKAWA usigharimu chembe ya damu ya vijana wetu. CCM na UKAWA wajibikeni katika hili. Mashindano ya kuingia ikulu yasitusababishie kupoteza maisha ya Mtanzania hata mmoja. Kwani ikulu itabaki ya wachahe na vijana mlio wengi maisha yatandelea yale yale kwa muda mrefu.
No comments: