Ushirikina Usihusishwe Na Misiba



Na Amb.Dr. Ahmed Kiwanuka

Kifo cha Dr. Emmanuel Makaidi ni msiba mkubwa kwa Taifa. Dr. Makaidi ni Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wanannchi UKAWA kupitia NLD atakumbukwa kwa sifa tatu tofauti; wanamichezo hasa wana Yanga watamkumbuka kama Simba Mkongwe, hakika kifo chake si msiba kwa UKAWA na NLD pekee bali kwa taifa letu.

Kabla hatujamaliza kutafakari, umetokea msiba mwingine mbunge kijana machachari Deo Filiku njombe, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa. Huu ni wakati wa kutafakari na kupeana pole. Jambo la muhimu tuwaombee wenzetu waliotangulia mbele za haki. Kwa hali ya kawaida waswahili wengi watasema kuna mkono wa mtu, huu ndiyo utamaduni wetu. Hata hivyo tukumbuke, kuzima kwa koleo sio mwisho wa uhunzi Deo Filiku njombe, Dr. Makaidi, Mchungaji Christopher Mtikila, Dr. Abdallah Kigoda, Waziri Celina Kombani, Estomih Malla, Mohamed Mtoi pamoja na viongozi wengine wametangulia Tanzania ipo tuendelee kuimarisha demokrasia. Ukweli utabakia, wamefariki jukumu letu ni kuwaenzi kwa kufanya uchaguzi wa amani na haki.



Marehemu Dr. Emmanuel Makaidi



Marehemu Deo Filiku



Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila



 Marehemu Dr. Abdallah Kigoda,



Marehemu Waziri Celina Kombani,

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger TemplatesPublished.. Blogger Templates